Witnesz Kibonge Mwepesi aeleza kwanini ametoka na ngoma inayokwenda kwa jina la Sharifa. 

Akiongea na chadonewz blog wiki moja iliyopita Witnesz amesema aliamua kuandika ngoma hiyo kuikumbusha jamii kwamba mtoto wakike naye ana haki ya kuthaminiwa na kusikilizwa ili atimize malengo yake ya baadae kwa kuwekewa misingi imara na jamii husika. 

Niliona nadhani mwaka jana bungeni waheshimiwa wakiwa na mivutano kuhusu haki ya mtoto wakike hasa ndoa za utotoni na kwakuwa tatizo hili ni kubwa kwenye jamii nikaona ni bora na mimi niliseme kwa njia hii ya muziki” alieleza. 

Mabinti wanaweza kufanya mambo makubwa yanayoweza kusaidia familia na Taifa pale wanapoandaliwa vizuri na mimi nimeguswa sana na hilo hivyo nikaamua kuieleza jamii kuhusu ukubwa wa tatizo na umuhimu wa kuliepuka”. 

Pig up sana Witnesz Kibonge Mwepesi kuimbuka jamii kwani kiuhalisia wasanii wengi wabongo hasa wa bongofleva kauli mbiu yao ni kwamba Mapenzi yanarun Dunia hivyo hata mashairi yao hulenga Mapenzi na Bata Mimi naona lipo jambo la kujifunza hapa kwa wasanii wetu Tz. Nimekuekea Wimbo huo hapa chini usikilize

0 comments:

Post a Comment

 
Top