NEWALA-MTARA Na; Sigfrid Bina 

Halmashauri za vijiji na wilaya nchini zimetakiwa kuunga mkono juhudi za Asasi za kiraia za kutetea haki za watoto na wanawake ikiwa ni njia ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia. 

Wito huo umetolewa na Msemaji wa Asasi ya kutetea haki za wanawake wilayani Newala mkoani Mtwara (NEWORA) Bi. Mwajuma Nambole wakati wa mahojiano maalum na chadonewz blog ofisini kwake mjini Newala kufuatia taarifa uliyotolewa wanahabari katika mafunzo ya siku mbili kutoka kwa Chama Cha Waandishi Wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) yaliyofanya wiki iliyopita wilayani Ruangwa mkoani Lindi. 

Katika mafunzo hayo ya siku mbili, wanahabari walibainisha kuwa kumekuwa na ushirikiano mdogo kati yao, wanajamii na serikari kwani matukio mengi ya namna hiyo yamekuwa yakiishia kusuluhishwa nyumbani kwa maelewano sambamba na upokeaji wa pesa ili kuyamaliza mambo hayo pasipo kufuata sheria za nchi kupitia vyombo vya dola. 

Hata hivyo katika mafunzo hayo imebainika kuwa wazazi wengi wamekuwa chanzo cha watoto wao kupata mimba za utotoni wakiwa shuleni kutokana kukosekana kwa malezi bora, kupenda kupokea zawadi kutoka kwa watoto na wanaume bila kutambua matokea yake, kitu ambacho ni hatari kwa ustawi wa maisha ya mtoto na kupunguza ushirikiano kwa vyombo vinavyosimamia sheria pindi tatizo linapojitokeza. 

Bi. Nambole amesema ili kufikia malengo ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia ni lazima halmashauri za vijiji na wilaya hapa nchini kuendeleza elimu inayotolewa kwa jamii kutoka kwa Asasi mbalimbali za kiraia. 
“Ujue tunafanyakazi kwa kutegemea wahisani hivyo tunakuwa na vipindi vipindi lakini tukimaliza elimu ile tunayoitoa haiendelei hivyo pindi tunaporudi tena tunaanza na moja na hiyo inatokana na halmashauri za Vijiji na Wilaya hazisaidii kuendeleza kile tunachokitoa kwa jamii” alisema 

Aidha msemaji huyo ameeleza kuwa, hali ya kikabiliana na vitendo vya unyanyasaji wakijinsia wilayani hapa bado hairidhishi kwani kumekuwepo na taarifa za kuendelea kwa matukio ya aina hiyo na jamii imeshindwa kuchukua hatua ya kudhibiti tabia hiyo kutokana na kuwa wasiri kwa kuficha ukweli wa matukio ya aina hiyo. 
Bi. Nambole amesema matukio mengi yanayojitokeza mara kwa mara ni ya ubakaji na talaka holela hivyo ipo haja ya kuangaliwa upya suala la ndoa na elimu ya uzazi wa mpango kwa jamii. 

1 comments:

 
Top