Klabu ya Soka ya Azam Fc wana-Lambalamba, yenye maskani yake Chamazi jijini Dar es salaam iliyokuwa inashiriki kombe la shirikisho barani Afrika hatua 16 bora usiku huu wametupwa nje ya michuano hiyo baada ya kukubali kichapo mabao 3-0.
Azam imepokea kipigo hicho kutoka kwa wapinzani wao, klabu ya Esperance ya Tunisia katika mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye dimba la Olimpiki Novemba 7 mjini Rades, Tunis mchezo ulioanza Saa 1:00 usiku kwa saa huko na Saa 3:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Dakika ya 44 Esperance walipata bao lililokataliwa na mwamuzi kwa madai ya mfungaji alikuwa ameotea hivyo ikalazimika timu hizo kwenda mapumziko kukiwa hakuna mbabe.
Mabao ya waarabu hao yalianza kupatikana mapema baada ya kipindi cha pili kuanza ambapo iliwachua dakika chache kuanza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 49 Saad Bguir aliipatia timu yake bao la kuongoza.
Mabao mengine yalipatikana katika dakika ya 62 mfungaji akiwa ni Haythem Jouini na bao la tatu likiweka nyavuni dakika ya 85 na kijana Ben Yousef hivyo kufanya ushindi wa 3-0.
Kufuatia matokeo hayo Azam imetupwa nje ya michuano hiyo kwa jumla ya Mabao 4-2 baada ya mchezo wao wa awali uliochezwa hapa Nchini katika dimba Chamazi Complex, Azam wakiwa walipata ushindi wa 2 -1.
Kikosi Cha Mwalimu Stewart Hall kilikuwa kimewakilishwa na
Aishi Manula, Erasto Nyoni, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Ramadhani Singano ‘Messi’, Frank Domayo, John Bocco, Salum Abubakar ‘Sure Boy, na Farid Mussa.
Azam katika mchezo walifanya mabadiliko ya kumpumzisha Farid Mussa na nafasi yake kuchukuliwa na Khamis Mcha, Sure Boy akampisha Himidi Mao na Waziri Salum nafasi yake ikachukuwa Didier Kavumbagu.
Yaani sisi timu zetu fuffu majivuno wacha wapigwe tu
ReplyDelete