G-Senior aelezea kwanini anaitwa Mr Real Love.
Akizungumza na Chadonewz blog G-Senior amefunguka na kusema jina hilo limekuja kutokana na ujio wa ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina hilo la Mr real love hiyo mashabiki wake wameamua kumbatiza jina hilo baada ya kuvutiwa na wimbo huo.
"Unajua kama mashabiki wako wakiamua kukutunuku kitu hauwezi kuwakatalia ikizingatia ni jambo zuri kuona watu wanakubali kile unachokifanya hivyo kwa kuwa mashabiki wameamua basi nitabaki kuwa mr real love nawapenda sana mashabiki zangu" amefunguka G.
Mr real love ni moja kati ya track zinazofanya vizuri hivi sasa ikiwa imefanywa katika mikono ya Producer Never Touch. Nimekuwekea ngoma yenyewe hapa chini isikilize na ipakuwe iwe yako.
0 comments:
Post a Comment